Chama
cha walemavu wa ngozi mkoa wa Mwanza kimepongeza hotuba ya rais
Mhe.Dr.Jakaya Mrisho Kikwete jana alipolihutubia taifa kupitia vyombo
vya habari akilaani ukatili dhidi ya mauaji ya walemavu wa ngozi hapa
nchini huku akivitaka vyombo vya kisheria kuwasaka hadi kuwakamata
watuhumiwa ili wafikishwe mahakamani na kupewa adhabu inayo wa sitahili
kwa lengo la kudhi biti mauaji ya albino yanayodhalilisha na
kufedhehesha taifa la Tanzania ambalo linasifika umoja wa mataifa kuwa
kisiwa cha amani.
Aidha rais Mhe.Dr.Jakaya Mrisho Kikwete katika hotuba yake
alisisitiza kuimalisha ulinzi hapa nchini na kukubali kukutana na
viongozi wa chama cha walemavu wa ngozi wiki ijayo kwa lengo la kutafuta
ufumbuzi wa kumaliza tatizo la mauaji ya albino ambapo mwenyekiti wa
chama cha albino mkoa wa Mwanza Bw.Alfred Kapole amempongeza rais kwa
kulaani mauaji ya albino na kusema kwamba endapo watendaji wa serikali
wakitekeleza agizo rais ukatili dhidi ya walemavu wa ngozi utapungua au
kukomeshwa kabisa.
Wakati huohuo balozi wa marekani hapa nchini Mh.Mark Chidless
amemtumia salam za lambilambi mgonjwa Bi.Ester Jonas aliyejeruhiwa
vibaya na watu wasiojulikana hali iliyoradhim kulazwa katika hospitali
ya rufaa Bugando jijini Mwanza na kumpa pole kwa kupoteza mtoto wake
kipenzi Yohana Bahati mwenye umri wa mwaka mmoja aliyetekwa nyara na
wahalifu kisha wakamuuwa na kutoweka na baadhi ya viungo vyake ikiwemo
mikono na miguu ambapo salam hizo zimewasilishwa na afisa usitawi wa
jamii wa shirika la kutetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania
Under the same sun Bi.Ester Rwela kwa niaba ya mkurugenzi wa shirika
Vick Ntetema na kusema kwamba balozi wa marekani amesikitishwa sana na
uhalifu unaotendeka dhidi ya walemavu wa ngozi na kuitaka serikali ya
Tanzania kuwachukulia hatuua za kisheria watuhumiwa wa mauaji ya
walemavu wa ngozi.
Wakiwashukuru wasamalia wema wa ndani na nje ya nchi Bi.Ester Jonas
na mama yake mzazi Bi.Tabu Maganiko baada ya kupokea msaada wa fedha
kiasi cha shilingi milioni moja kutoka ITV, Radio One zilizotolewa na
mfuko wa hifadhi ya jamii GEPF ambapo katika kipindi cha wiki mbili
zaidi ya shilingi milioni saba zimepatikana kutokana na misaada ya watu
mbalimbali wa ndani na nje ya nchi huku wakiomba mashirika na taasisi
kuwasaidia kulea watoto wawili wa Ester Jonas walemavu wa ngozi ambao
wanaishi kwa hofu kubwa hoko kijijini baada ya mdogo wao kuuwa wa
kinyama.