Askari magereza aliyekutwa na noti bandia afukuzwa kazi



JESHI la Magereza nchini, limemfukuza kazi askari wake wa Gereza la Bariadi, mkoani Shinyanga kwa kosa la kupatikana na fedha za bandia kinyume cha sheria.
 
Taarifa iliyotolewa jana na Mkaguzi wa Magereza, Lucas Mboje na kusainiwa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Minja, ilimtaja askari huyo kuwa ni Namba B. 6499 Wdr. Edmund Masaga.
 
Alisema askari huyo amefukuzwa kazi kwa fedheha kuanzia Machi 28 mwaka huu kwa kosa la kulidhalilisha jeshi hilo kinyume na Kanuni za Utumishi wa Jeshi la Magereza za mwaka 1997.
 
Katika taarifa hiyo, Kamishna Jenerali Minja alikemea vitendo hivyo ambavyo alisema ni kinyume cha maadili na utendaji ndani ya Jeshi la Magereza.
 
Hata hivyo aliwataka askari wote nchini kutenda kazi zao kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.
 
Wiki iliyopita polisi mkoani Simiyu liliwakamata askari wawili wa jeshi la magereza baada kukutwa na noti bandia ikiwa ni pamoja na sare za jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ).
 
Akitoa taarifa za kukamatwa kwa askari hao, Kamanda wa polisi mkoani humo, Naibu Kamishina, Charles Mkumbo alisema askari hao walikamatwa saa 9 mchana katika Mtaa wa Old Maswa Kata ya Nyakabindi wilayani Bariadi.
 
Baada ya askari hao kukamatwa mmoja wao, PC Juma alipopekuliwa katika mfuko wa suruali yake alikutwa na noti nyingine za bandia za elfu kumi na jumla yake kama zingelikuwa halali zingelikuwa na thamani ya Sh 1,920,000.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo