AIBU HII KUHUSU KISHA CHA MWANAUME KUGOMBANIA MTOTO

HMIcontrol2Hekaheka ya leo March 4, inahusu mvutano wa mtoto anaegombaniwa na wanaume wawili huku kila mmoja akidai ni mtoto wake baada ya mama yake kufariki.

Mama wa hiari wa familia ya mwanaume mzungu amesema kuwa aliwahi kupata malalamiko kutoka kwa mke wa mzungu kuwa mume wake ana mwanamke wa kiswahili na amezaa nae mtoto ambae alikuwa akija nyumbani kwake mara kwa mara akiwa na mama yake hadi walipohama na kurudi Togo, baada ya mwanaume huyo kusikia mama wa mtoto huyo amefariki akarudi Tanzania kuja kumchukua walimkatalia na kumwambia sio mtoto wake.

Mama wa kijana wa kiarabu anaedai kuwa baba halali wa mtoto huyo amesema, kijana wake alikuwa na mahusiano na huyo binti lakini alipogundua anamahusiano na huyo mzungu aliamua kuachana nae, wakati huo tayari alikuwa na ujauzito wake baade aliambiwa mtoto huyo sio wakwake lakini hakukubali wakamtaka wapime DNA jambo ambalo alikataa na kupeleka swala hilo Polisi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo