Kijiji cha Igolwa kilichopo katika kata ya Ipepo tarafa ya Lupila wilayani Makete kinakabiliwa na tatizo la ukosefu wa huduma ya afya kutokana na kutokuwepo kwa wahudumu wa kutosha katika zahanati ya hicho.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wananchi hao mbele ya Mkuu wa wilaya Mh Josephine Matiro ni kwamba kituo hicho si cha serikali bali ni mali ya kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) ambapo kwa mara ya kwanza walipotoa lalamiko hilo halmashauri ya wilaya ya Makete iliwapa muuguzi mmoja.
Aidha wamedai kuwa hadi sasa muuguzi huyo hayupo kituoni hapo kwa muda mrefu kutokana na sababu zisizozuilika na kuwafanya wananchi hao kukosa huduma hiyo na kulazimika kufuata huduma hiyo katika hospitali ya Consolata Ikonda.
Aidha wameongeza kuwa kutokana na kukosekana kwa huduma hiyo baadhi yao hushindwa kufuata huduma kutokana na umbali mrefu na gharama za usafiri kuwa kubwa,ambapo hadi sasa nauli kwa usafiri wa boda boda ni kati ya 15,000 - 20,000 kwa kwa safari ya kwenda tu, hivyo kwenda na kurudi huwalazimu kulipa sh.30,000 hadi 40,000.
Kwa upande wake Kaimu Afisa mtendaji wa kata cha Igolwa Percy Sanga amekiri kuwepo kwa tatizo hilo, ambapo amesema alipopeleka waraka kwenye halmashauri ya (w) ndipo walipopewa muuguzi mmoja huku wananchi hao wakiomba zahanati hiyo ibadilishwe umiliki na kuwa mali ya serikali.
Mkuu wa wilaya Mh. Josephine Matiro alipokuwa akijibu changamoto hiyo amesema kuwa anamwagiza Afisa mtendaji huyo kuandaa waraka maalumu kuhusu tatizo hilo pamoja na kuandaa taratibu za kujenga zahanati ya serikali kwa nguvu zao wenyewe na serikali itamalizia sehemu iliyobaki kwani suala la kuibadilisha na kuwa milki ya serikali sio jambo rahisi na la haraka.
Kwa upande wa wazee na vikongwe pia wamelalamikia utolewaji wa huduma hiyo kutopatikana kwa urahisi katika eneo hilo kwani hulipia huduma hiyo licha ya serikali kutangaza wazee watapata huduma ya matibabu bure.
;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;