WASIFU WA MHE. AWADH ALIYEFARIKI GHAFLA JANA ZANZIBAR!

Mwili wa marehemu, Salmin Awadh ukiwekwa kwenye gari ukitolewa kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja kwenda nyumbani kwake kwa matayarisho ya mazishi.

Mwakilishi wa jimbo la Magomeni, Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Salmin Awadh  amefariki dunia ghafla Jana akiwa katika Kikao cha Kamati Kuu Zanzibar, katika ofisi kuu ya chama, Kisiwandui.

Mheshimiwa Awadh alizaliwa Juni 26 mwaka 1958 na alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Makunduchi na Kiongoni kati ya mwaka 1963-1970.

Marehemu aliwahi kufanya kazi katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania akiwa na cheo cha Sajenti kati ya mwaka 1976 hadi 1986.

Hadi wakati mauti yanamkuta alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Gazeti la Zanzibar Leo, nafasi aliyokuwa nayo tokea mwaka 2009.
Mwakilishi wa jimbo la Magomeni, Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Salmin Awadh enzi za uhai wake.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo