Mwenyekiti huyo wa TWPG amesema hayo katika Mafunzo maalumu ya baadhi ya wabunge walioteuliwa juu ya hedhi salama kwa watoto wa kike ambapo wabunge hao wametunikiwa ubalozi kuhusu elimu hiyo.
Bi Magreth Sitta amesema kuwa serikali ina wajibu wa kipekee katika kufikisha elimu kwa watoto wa kike huku wabunge wangine wakimuunga mkono juu ya jitihada za serikali katika kufanikisha azma hiyo.
"Kidunia wameona hili jambo linaweza kujadiliwa kwa kutumia lugha nzuri na watu wakaelewa kwamba jinsi gani mtoto wa kike anashindwa kwenda shule kutokana na zile siku anazoingia kwenye siku zake. Serikali inabidi itusaidie kupambana na hili suala la hedhi, wanafunzi wanashindwa kwenda shuleni kutokana na mazingira yalivyo. kwamaana kupunguza kodi kwenye vifaa vya kujisitiri" Bi Sitta.
Aidha wabunge mbalimbali wameunga mkono hoja hiyo kwa kuitaka serikali iliangalie suala hili kwa undani kwani kwa makadirio ya watoto wa kike kushindwa kwenda shuleni kwa mwaka mzima lazima ufaulu wake utakuwa chini kwa mtoto wa kiume.
Wiki iliyopita Mbunge wa kuteuliwa upendo Penneza alijaribu kupeleka hoja binafsi kuhusu wanafunzi wa kike kupatiwa pedi lakini hoja hiyo haikufanikiwa kwani hoja hiyo ilikataliwa kwa sababu yakuwa inavunja ibara ya 99 (2) ya Katiba.