Serikali imeruhusu wanafunzi wa shule za msingi na sekondari waliopata ujauzito kuendelea na masomo wanapojifungua.
Mratibu
wa Masuala ya Jinsia wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Chimpaye Marango, wakati wa mjadala wa sababu za kuongezeka kwa idadi ya
watoto ya mabinti wanaokosa elimu baada ya kupata mimba.
Mjadala huo ulioitishwa na asasi ya kiraia ya uchambuzi wa sera ya Policy Forum iliwakutanisha wadau mbalimbali wa elimu.
Marango
alisema lazima wasichana waliopewa ujauzito kuhakikisha wanarudishwa
haraka shuleni mara watakapojifungua, vinginevyo hatua kali
watachukuliwa watakaowazuia.
“Wizara
imeliona hilo na tayari imewekwa sera mpya, kwani kumuadhibu kwa
kumfukuza shuleni hakutaweza kuwasaidia watoto wa kike kumudu maisha
badala yake tunaongeza umasikini ndani ya jamii,” alisema Marango.
Awali,
Dk. Rebecca Balira, kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Tiba Afrika
(Amref) alisema tatizo la mimba kwa wanafunzi wa kike limekuwa sugu
nchini.
Alisema
katika utafiti uliofanyika katika Wilaya za Kilindi, Mkalama, Iringa
vijijini na Same jumla ya wanafunzi wa kike 55,000 walishindwa
kuendelea na masomo kwa kipindi cha mwaka 2003 hadi 2011.
Dk.
Balira alisema kwa upande wa shule za sekondari kwa muda wa miaka
mitano inayoishia 2011 idadi ya wanafunzi waliopata mimba ilipungua
kutoka asilimia 21 hadi 6.7.
Kwa
upande wa mwakilishi kutoka vyama vya kiraia, Mariam Asha , alisema
kunahitajika juhudi ya kutoa elimu ya afya ya uzazi kuanzia ngazi ya
shule ya msingi kutasaidia wanafunzi wajitambue na kukabiliana na
vitendo hatarishi.