Kuna
matukio ambayo huwa yanachukua headlines kubwa kwenye vyombo vya habari
kutokana na sababu mbalimbali, mengine sio ya kawaida kuyasikia na
lazima ishu kama hii utajiuliza mara mbilimbili chanzo ni nini.
Mwanamke mwenyewe anaitwa Catherine Muthoni, tukio limetokea Nairobi Kenya ambapo alimuua mtoto
wake wa siku tano kwa kumchinja, akautoa moyo wake na kuula kabla ya
kuingia kwenye nyumba ya jirani na kunyonga Mwanamke mwenzake ambae hata
hivyo alifanikiwa kumchoropoka na kuwaacha watoto wake wawili.
Kituo cha TV cha K24
kimeripoti kwamba baada ya jirani huyo kukimbia, Catherine alianza
kuwafata Watoto wawili wa jirani yao ili awaue lakini Wananchi
walimuwahi na kumzidi nguvu.
Baadae alikamatwa na Polisi na mpaka
sasa anashikiliwa huku uchunguzi ukiendelea, mashuhuda wanahusisha tukio
hilo na imani za kishirikina kwamba huenda Catherine ni mfuasi wa dini
zinazomuabudu Shetani.