Moja ya story ambazo ziliwahi kuchukua
headlines ilikuwa ya mwanamke ambaye alijifungua akiwa safarini kwenye
ndege akitokea Jordan kwenda Marekani.
Mwanamke mmoja kutoka Rajastan, India alikuwa
akisafiri na mume wake pamoja na mama yake kutoka Suratgarh kwenda
Hanumangarh kwa treni, alishikwa na uchungu wa kujifungua wakati akiwa
anajisaidia kwenye choo ndani ya treni hiyo, kwa bahati mbaya mtoto huyo
akateleza na kuanguka chini kwenye reli kupitia kwenye jomba la kutolea
maji machafu kutoka kwenye choo hicho.
Mfanyakazi wa treni hiyo alisikia mtoto
huyo akilia akatoa taarifa kwa kiongozi ambapo walimchukua mtoto huyo
pamoja na mama yake wakawapeleka Hospital.
Kwa mujibu wa daktari kutoka Hospitali
walipokuwa wakitibiwa mtoto huyo pamoja na mama yake amesema hali zao
wote wanaendelea vizuri.