Mwanamke mmoja Kenya amefariki baada ya
kuanika nguo katika nyaya za senyenge zilizokuwa zimeshikana na nyaya
za umeme zilizokuwa zimekatika karibu na mto ambao wanachota maji.
Wakazi wa eneo hilo wamesema
hawakujua kama nyaya hizo za umeme zilikuwa zimegusana na nyaya za fensi
ya kuanikia nguo na matukio kama hayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa
mara na kuomba Shirika la Umeme Kenya kuondoa nyaya hizo.
“Sababu
ni mara nyingi sana shida ikitokea kule chini inapigiwa simu.. kwanza
iling’oa miti ikachoma forest huku chini… waya ulikatika na wakati yule
mzee alikuwa anasema hizo waya zilishikana alafu zikatetemesha nyumba
yote“– alisimulia shuhuda huyo.