Jana katika kikao cha Bunge Dodoma,
kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu moja ya swali ambalo liliulizwa ni
ishu ya chama cha CCM kuwatumia wanafunzi katika sherehe za chama hicho
zilizofanyika Songea mwisho wa wiki iliyopita.
“Tumeambiwa
kwamba tustumie wanafunzi kushiriki katika masuala ya kisiasa hasa
katika vyuo na mashule. Hivi karibuni mkuu wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na
viongozi wa Ruvuma wamewatumia wanafunzi wa Manispaa ya Songea kushiriki
katika maamuzi ya miaka 38 ya Chama cha Mapinduzi… Kwa nini msitumie
wanachama wenu kwenye sherehe hizo mnaenda kutumia wanafunzi”— Susan Lyimo.
“Unajua
mtoto wa nyoka ni nyoka, chama kina mfumo wake ambao umeshuka mpaka
kwenye ngazi ya kitu kinaitwa chipukizi, ni watoto ambao wamezaliwa
kutokana na wazazi wana CCM ndio maana chama kiliwatumia. Wao
walichokuwa wanafurahia pale ni ile parade na kuonekana wamepiga sare
ile basi…”—Waziri Mkuu Pinda.
“Nimesikitishwa
sana na ajibu ya Waziri Mkuu. Pamoja na watoto hao kuwa wadogo lakini
utatambua kwamba baadhi ya watoto hawa vilevile wazazi wao ni wanachama
wa vyama vya upinzani, sikubaliani na wewe kwamba watoto hawa wazazi wao
ni wa chama cha mapinduzi…” Mbunge Susan Lyimo.
“Na mimi naheshimu sana maelezo ya mama Susan… Kiachieni chama na utaratibu wake waendelee nao mimi sioni kama kuna tatizo…”—Waziri Mkuu Pinda.
“Waziri
Mkuu amehararisha jambo ambalo nikinyume na haki za binadamu…
kuwalazimisha watu kwenda kwenye shughuli, tuna barua ambayo Mkuu wa
Mkoa alimwandikia Afisa Elimu kuwalazimisha vijana wa Songea Boys na
Songea Girls wavae sare za CCM na walimu waende kule kwa lazima …
Mwongozo wangu ni kwamba Waziri Mkuu afute kauli hapa”—Felix Mkosamali.
“Wale
watoto waliambiwa waombe wenyewe, jioni saa kumi baada ya masomo yao
nd’o walifanya gwaride lile sio wakati wa kazi n ahata sherehe yenyewe
imefanyika siku ya jumapili ambayo sio siku ya kazi…”
Unaweza kusikiliza mjadala wote juu ya ishu hiyo kutoka Bungeni kwa kubonyeza play hapa