Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na
mwenyeji wake Rais wa Zambia Edgar Lungu pamoja na wake zao Mama Salma
Kikwete na Mama Esther Lungu wakinyanyua glasi juu wakati wa dhifa ya
kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake ambao
walifanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Zambia.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na
mwenyeji wake Rais Edgar Lungu wa Zambia wakigonga glasi wakati wa dhifa
ya kitaifa aliyoiandaa kwa heshima ya Rais Kikwete jijini Lusaka Zambia
jana jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akigonga glasi na Rais wa Kwanza wa taifa la Zambia Dkt.Kenneth Kaunda
wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete
jijini Lusaka Zambia jana jioni.Rais Kikwete ambaye alikuwa katika ziara
ya siku mbili nchini Zambia tayari amerejea jijini Dar es Salaam. (picha na Freddy Maro)
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini
Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Zambia kwa
ajili ya mazungumzo rasmi na Mwenyeji wake Rais Edgar Lungu ( mwenye
suti ya kijivu aliyesimama mbele ya Rais Kikwete).
|
Rais Lungu akimkaribisha Rais Kikwete (hayupo pichani kuzungumza).
|
Mhe.
Rais Kikwete akizungumza wakati wa mazungumzo rasmi na Rais Lungu na
Ujumbe wake katika Ikulu ya Zambia. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe na kulia ni Waziri wa
Fedha, Mhe. Saada Mkuya Salum na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe.
Grace Mujuma.
|