Baada ya wapangaji hao kushtuka kwamba
wanafanyiwa utapeli mmoja wao alimkamata mwenye nyumba huyo na kumpeleka
Kituoni hapo, amekaa kwa zaidi ya wiki moja huku wakipewa taarifa na
askari kwamba madeni ya wapangaji hao inakaribia milioni 40 na mwenye
nyumba huyo hana hela kuwalipa wote wanaomdai.
Picha hii imewekwa na Geah Habib katika ukurasa wake Instagram, kinachoonekana hapo ni ‘mwenye nyumba’ huyo, nyumba yake na mkataba wa mpangaji mmoja aliyetapeliwa.
Majirani wa nyumba hiyo wamesema kuwa
hiyo nyumba ni ya urithi ambayo ndugu wamegawana vyumba na kupangisha
lakini huyu amekuwa na tabia ya utapeli na pia ana tabia ya kuwaibia
wapangaji wake ambao tayari wanaishi hapo, anawapa funguo moja moja za
milango halafu nyingine anabaki nazo, wakiwa hawapo anafungua na
kuwaibia.