Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imeingilia kati tukio la mwalimu wa Sekondari ya Kibasila, Gaudensia Albert kukaa na kinyesi ,mende na funza ndani kwa muda wa miaka miwili na kutaka kumchukulia hatua.
Ofisa Afya Manispaa ya Temeke Willium
Mihemu alisema kwa sasa yupo kwenye mikakati ya kujiandaa kushirikiana
na na askari polisi kumchukulia hatua mwalimu huyo anayefundisha masomo
ya sayansi hapo shuleni.
“Leo sisi na Polisi tutaungana ili kwenda kumkamata,kwani kwa hali ya kawaida inaonekana mwalimu huyo hana akili timamu“-Mihemu.
Kwa upande wa mwenye nyumba Ruben Shayo
ambaye wanaishi eneo la Yombo Visiwani alisema kuwa licha ya kufanya
tukio hilo kwa miaka miwili mfululizo lakini bado alimruhusu kuendelea
kuishi ndani ya nyumba yake na kumtaka kuondoa kinyesi hicho.
Shayo alisema hajawahi kumuona mwalimu
huyo akimwingiza mgenindani ya nyumba hiyo badala yake alikua
akimalizana nao nje ya chumba chake.