Hekaheka ya February 02 inatokea
Magomeni Dar inahusu tukio la mauaji lililotokea katika Hoteli moja
maeneo ya Magomeni Kagera ambapo mtu mmoja alifika kwenye Hoteli hiyo na
kufanya mauaji.
Mhudumu wa Hoteli hiyo amesema wateja
hao walilipia chumba kwa siku moja na kesho yake mwanaume huyo
aliwaambia kuwa anaendelea kuwepo hotelini hapo, baadae wahudumu
walimgongea mlango ili alipie chumba lakini mteja huyo aliwaambia kuwa
hafungui mlango hadi Polisi waje.
Wahudumu waliamua kumchukua mtu mmoja
ambaye alijifanya Polisi wakaenda kumgongea mlango, alipofungua
wakakuta damu zimetapakaa kwenye chumba hicho.
Baada ya kukuta hali hiyo walitoa
taarifa Polisi ambapo walifika na kukumkuta bado yuko ndani na
walipomuuliza alisema kuwa amemuuwa mke wake, huku na yeye akiwa na
majeraha yanayosemekana kuwa alitaka kujiuwa mwenyewe.
Ndugu wa mtuhumiwa huyo amesema kuwa
aliyeuawa ni mke wa ndoa wa mtuhumiwa huyo, walikuwa na ugomvi muda
mrefu uliosababisha waishi tofauti, mtuhumiwa amekiri kumuua lakini
hakutoa sababu ya kufanya mauaji hayo, kwa sasa anashikiliwa kituo cha
Polisi Magomeni.
Bonyeza play kusikiliza Hekaheka yote hapa.