Viongozi wa dini wameshauri majangali
watakaokamatwa na kuthibitika kufanya ujangili, wang’olewe meno ili
wasikie uchungu wa kufanya vitendo hivyo kwa wanyama.
Aidha alionya ni wakati kwa waovu hao
kufika mwisho na kuacha ujangili wa kuua wanyama na kuchezea rasilimali
nyingine za nchi bila kuchukua hatua.
Baddhi ya viongozi hao wadini walionya
kulegalega kwa viongozi wa Serikali na kushindwa kukabiliana na ujangili
na kwamba hali hiyo ni kuwadanganya wananchi katika jambo kubwa
linalohusu uchumi wao.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Alhad Musa Salum alisema umefika wakati wa viongozi wa dini kujitokeza
waziwazi na kuisaidia Serikali katika vita dhidi ya ujangili.
Askofu Joseph Mwingira alisema Serikali
ina dhamana ya kulinda rasilimali kama itasimamiwa vizuri ujangili
utaisha na umaskini nao utaisha.