skip to main |
skip to sidebar
AJALI YA GARI: WATATU WANUSURIKA KUFA KWA AJALI MWANZA
Mwonekano wa gari hilo baada ya kupata ajali.
Wasamaria wema wakitoa msaada.
Mashuhuda wakiwa katika eneo la tukio.
GARI dogo aina ya Toyota RAV4 limepinduka leo
katika kijiji cha Mbela wilayani Misungwi, mkoani Mwanza na kujeruhi
watu kadhaa waliokuwa ndani yake baada ya kumshinda dereva wake wakati
lilikata kona na hivyo kuanguka katika bonde la daraja.
Kwa mujibu wa mashuhuda, gari hilo lenye usajili wa T 358 CBA mali ya
Machalo Joseph, lilikuwa likiendeshwa na Festo Kakula wa Misungwi, na
baada ya ajali majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya Mitindo
wilayani Misungwi.
CREDITS GPL
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi