Inaelezwa kuwa akina mama wanaojifungua watoto hao
na kwa bahati mbaya kupoteza maisha, viungo vya watoto hao huwa havipelekwi
kuzikwa kama ilivyo kawaida na taratibu za hospitali, badala yake wauguzi na
wafanyakazi wengine huchukua viungo hivyo na kupeleka kwa waganga wa jadi.
Tuhuma
hizo zilitolewa juzi mbele ya Katibu Tawala
wa Mkoa wa Simiyu, Mwamvua Jilumbi katika kikao cha pamoja na wadau wa
afya mkoa
kilichofanyika katika ukumbi wa kanisa la KKKT mjini Bariadi
wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa kukomesha vifo vya wajawazito
na watoto mkoani Simiyu ulioko chini ya AMREF Tanzania.
na watoto mkoani Simiyu ulioko chini ya AMREF Tanzania.
Wadau hao walibainisha kuwa hali hiyo imekuwa
ikijitokeza kila mara katika hospitali ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, ambapo
walieleza kuwa mtandao mzima wa kuuzwa kwa viungo hivyo ufanyika kati ya
wauguzi pamoja na madaktari ambao ndiyo wahusika wakuu kuzalisha akina mama
wajawazito.
Mbele ya Katibu huyo tawala wa Mkoa wadau hao
waliendelea kueleza kuwa viungo hivyo vimekuwa vikiuzwa kuanzia shilingi
400,000 hadi 500,000 kiasi ambacho walieleza hutolewa na waganga wa hao wa jadi.
“..katika hospitali yetu ya Bariadi kuna jambo
ambalo siyo zuri na jema leo ngoja tulitoboe mbele ya kikao hiki na tena mbele
za waandishi wa habari na wewe Katibu tawala wa Mkoa..akina mama wanaojifungua
watoto wao kwa bahati mbaya akafariki viungo vya watoto hao huuzwa kwa waganga
wa jadi” Alisema Gasper Mathew na kuongeza kuwa..
“ viungo hivyo vinauzwa shilingi 400,000 hadi
500,000 huu ni ushirikina wa hali ya juu na ni hatari..wauguzi pamoja na
madaktari ndiyo wanahusika sana..wamekuwa wakipewa kiasi hicho..kila mara
wanafaya hivyo lakini tumekuwa kimya” Alisema
Walisema
kuwa akinamama wengi hufika
hospitalini hapo kwa lengo la kujifungua na mara wanapojifungua na kwa
bahati mbaya mtoto au watoto kufariki kutokana na matatizo ya afya ya
uzazi baadhi huamua kuwahifadhi
katika chumba cha maiti lakini wengi hujikuta wakirejea nyumbani mikono
mitupu
baada ya miili ya watoto wao kuuzwa kwa waganga wa kienyeji.
Akizungumzia tuhuma hizo Katibu Tawala wa Mkoa wa
Simiyu,Mwamvua
Jilumbi katika kikao hicho alimtaka Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji wa Bariadi Erica Mssika kutoa maelezo juu ya tuhuma hizo.
Jilumbi katika kikao hicho alimtaka Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji wa Bariadi Erica Mssika kutoa maelezo juu ya tuhuma hizo.
Akitoa maelezo ya tuhuma hiyo Mkurugenzi huyo
alisema kuwa hana taarifa yoyote juu ya kuwepo kwa vitendo hivyo katika
hospitali yake, huku akieleza kuwa watafanya uchunguzi mara moja na watakao
bainika kufanya hivyo watachukuliwa sheria mara moja.
“..hii ni hatari mimi hili nimelipata hapa na
nimelisikia leo sina taarifa yeyote.. ila nawaomba wadau waliotoa tuhuma hizi
tushirikiane tufanye uchunguzi haraka ili tuwabaini na watakaobainika
tutawachulia sheria za kinidhamu” Alisema Mssika.
Katika kikao hicho Meneja Mradi wa Shirika lisilo
la kiserikali linalojihusisha na masula ya afya AMREF Health Africa tawi la Tanzania,katika
mkoa wa Simiyu, Godfrey Matumu, aliitaka jamii ya mkoa wa Simiyu
kushiriki kikamilifu katika kuthibiti vifo vya akinamama wajawazito na watoto
wachanga wenye umri chini ya miaka mitano.
Alisema vifo hivyo vimekuwa vikisababishwa
na kuchelewa kupata huduma katika vituo vya afya kwa wakati.wakati wa kuzindua
Mpango Mkakati wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto katika mkoa wa Simiyu utakaotekelezwa
kwa muda wa miaka 4 (2014-18),chini ya msaada wa watu wa Canada.
Chanzo-http://simiyunews.blogspot.com