Jeshi la Polisi kanda maalum ya DSM limepiga marufuku maandamano ya vijana wa CUF yaliyokuwa yafanyike LEO Feb 13

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya jumuia ya vijana wa chama cha wananchi CUF yaliyokuwa yafanyike Feb 13 mwaka huu.

Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari amesema .
 
hata hivyo licha ya jeshi la polisi kupiga marufuku maandamano hayo vijana hao wamesisitiza kuwa maandamano yao ya kuitaka tume ya uchaguzi kuongeza siku za kuandikisha daftari la kudumu la wapiga kura yanayotarajiwa kufanyika Feb 13 yako palepale.
 
Mwenyekiti wa JUVICUF taifa Bw Hamidu Bobali ameyasema hayo jijini Dar es Salaam ambapo amesema maandamano yao mbali na kuishinikiza tume kuongeza siku za kujiandikisha pia yana lengo la kulani ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi la polisi nchini na kuongeza kuwa hawawezi kusitisha kutokana na hoja wanazotaka kuwasilisha zina maslahi mapana kwa taifa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo