Watu
watatu wamefariki dunia kwa kuungua moto hadi kuteketea kabisa
akiwemo dereva na utingo wake baada ya lori la mafuta kuacha njia na
kupinduka na kuungua moto katika eneo la Maseyu barabara ya Morogoro Dar
es Salaam.
Blog hii imeshuhudia kikosi cha zimamoto ambao walichukua muda kuuzima
moto huo kutokana na kusamabaa ambapo hata hivyo hakukua na matukio ya
watu kujitokezakuiba mafuta kama ilivyozoeleka.
Baada ya kumaliza kuuzima moto huo hapa kikosi cha zimamoto na
uokoaji wakafanya juhudi nyingine za kuvuta kwa craine ili na kukata kwa
kutumia mashoka mabaki ya lori hilo baada ya walioshuhudia tukio hilo
kueleza kuwa watu wote waliokuwemo katika gari hawakutoka ambapo baada
ya muda miili mitatu iliokolewa ikiwa imuungua kabisa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo maderva wa malori
ambapo walikua wakisafirisha mafuta katika kampuni moja Farhan Yusufu
amesema lori hilo lilikua limesheni mafuta ya Dezel mali ya kampuni ya
Petro Africa ilikua ikitokea Dar es salaam kwenda jijini Mwanza ambapo
ilipoteza uelekeo na kupinduka kisha kuwaka moto ambapo waliofariki
dunia ni Ahmed Dilie dereva na utingo wake aliefahamika kwa majina ya
Emela na mtu mmoja ambaye bado hajaweza kufahamika mara moja.
Nao wananchi walishuhudia tukio hilo wameeleza jinsi tukio
lilivyotokea ambapo wananchi wamelalamikia eneo hilo limekua na matukio
mengi ya ajali na hivyo kuomba serikali kuona umuhimu wakuweka vituo vya
zimamoto katika eneo hilo kwani magari ya zimamoto yalichukua muda
mrefu kufika kwneye enelo la tukio kutokana na umbali mrefu.
Nae afisa mkaguzi msaidizi wa kikosi cha zimamoto Hamadi Dadi
ameeleza walivyopata taraari za ajali wametumia muda mrefu kufika katika
eneo la tukio ingawa wametumia muda mrefu kuzima moto huo kutokana na
mafuta yaliokua yakivuja.
Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na askari walionekana muda wote kwenye eneo la tukio.