ALBINO AMTOA MACHOZI MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL

Makamu wa  Rais Dr.Mohamed Gharib Bilali amelaani vikali vitendo vya mauaji na kudhuru watu wenye ulemavu wa ngozi yaani albino na kusema kuwa serikali inawasaka wahusika wa vitendo hivyo na pindi itakapowakamata itahakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe funzo kwa wengine.

Akizungumza kwa hisia kali katika maadhimisho ya siku ya Skauti duniani Dr.Bilali amesema vitendo hivyo havivumiliki kamwe na vimekuwa vikiitia doa Tanzania kwa kuonekana kuwa vinara wa imani potofu ya kuwa viungo vya mwanadamu kuwa mtaji wa utajiri kitu ambacho hakipo katika nchi yoyote ile Duniani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo