Majitaka
yenye Sumu hatarishi kutoka Kiwanda cha
Nguo cha 21st Century yakitiririka kuingia Mto Ngerengere, Mkoni
Morogoro ambapo Wanachi hutumia maji
ya Mto huo kwa matumizi ya nyumbani.
(Picha na OMR)
Majitaka
yenye Sumu hatarishi kutoka Kiwanda cha
Nguo cha 21st Century yakitiririka kuingia Mto Ngerengere, Mkoni
Morogoro ambapo Wanachi hutumia maji
ya Mto huo kwa matumizi ya nyumbani.
(Picha na OMR)
Na Victor Mariki – Ofisi ya Makamu wa
Rais
Baraza la Taifa la Hifadhi
na Usimamizi wa Mazingira, limetoa amri ya
kfungwa shughuli za uzalishaji
katika Kiwanda cha nguo cha 21st
Century Limited kilichopo Kihonda Mkoani Morogoro leo ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira.
Hatua
hiyo imechukuliwa kufuatiwa na
kupuuzwa kwa maelekezo na maagizo ya
mazingira yaliyokuwa yakitolewa nyakati
tofautit tofauti na Ofisi ya Makamu wa
Rais, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Morogo .
Kiwanda
hicho chenye wafanyakazi 1779 kiliagizwa na kuelekezwa tangu mwaka 2006 mamlaka
hizo kutumia mitambo ya kutibu majitaka
yake kabla ya kuyatiririsha kwenye Mto Ngerengere ili kuhepusha jamii inayotumia vyanzo vya maji
hayo na madhara ya kiafya.
Aidha
Taarifa ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ilifafanuwa
kuwa mitambo ya kutibu sumu ya majitaka
kiwandani hapo haina uwezo wa
kutosha kutibu sumu zinazozalishwa na shughuli za uendeshaji wa kiwanda hicho.
Taarifa
hiyo iliongeza kuwa kufungwa kwa kiwanda hicho ni sehemu ya Utekelezaji wa
Sheria ya Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004 pamoja na Kanuni za Mazingira ya mwaka
2007 ambazo zinavitaka viwanda kutibu majitaka yake hadi kufikia viwango
vilivyowekwa kabla ya kumwaga au kutiririsha maji hayo kwenye mazingira.