Familia tatu zalazimika kulala nje siku saba baada ya nyumba kuwaka moto mara kwa mara Morogoro

Katika hali  isiyo  kuwa  ya  kawada  familia tatu zenye  watu  16  katika kijiji cha Mikese mkoani Morogoro wanalazimika  kulala nje kwa siku saba mfululizo baada  ya nyumba wanazoishi  kuwaka moto  mara kwa mara na kuunguza thamani  za ndani  na  vyakula huku chanzo cha moto  hakifamahamiki   na kusababisha   hofu kwa familia hizo kutaka kuyakimbia makazi yao.

Blog hii ilifika katika familia hizo na kuona vitu mbalimbali vilivyoungua moto vikiwemo vyakula nguo madaftari ya wanafunzi  huku wakinamama na watoto  pamoja na wazee  wakiwa nje ambapo wamesema katika hali isiokua ya kawaidia moto huo huwaka  zaidi ya mara tisa kwa siku na wanajaribu kuuzima  lakini chanzo cha moto huo hakieleweki  ingawa nyumba hizo hazina umeme wala nishati ya aina yoyote  inayosabaisha moto ambapo wamefananisha tukio hilo kama la miujiza na kuomba watu wenye  imani  mbambali kufika na kufanya maombi katika nyumba hizo kwani wanateseka kwa kushindwa  kulala ndani.
 
Nao viongozi wa serikali yakitongoji cha lukole  katika eneo la tukio hilo mwenyekiti   Ramadhani  Shaban amekiri  kuwemo kwa matukio ya moto  kuwaka katika nyumba hizo kwa siku saba mfululizo ambapo amesema  si tukio la kawaida najitihada wanazozifanya kama serikali ya kijiji  wameanza kuwatafuta  wachungaji na mashekhe ili   kusaidia kufanya maombi katika  nyumba hizo kwnai familia hizo zinaishi katika mazingira magumu ya kulala nje kwa muda mrefu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo