Wafuasi 29 wa CUF Waachiwa kwa dhamana


WAFUASI 29 kati ya 30 waliokuwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam wameachiwa leo baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
 
Wafuasi hao walikamatwa majuzi huko Mtoni Mtongani, Dar wakati Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba akielekea Mbagala kuwataka wananchi watawanyike baada ya maandamano ya chama hicho kuzuiliwa na jeshi la polisi.
 
Wafuasi hao 29 wameachiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar baada ya kila mmoja wao kutimiza masharti ya dhamana kwa kutoa kiasi cha shilingi 100,000 pamoja na barua ya mdhamini mmoja ambaye hana hatia.
 
Mpaka mwandishi wetu anatoka eneo hilo la mahakama, mmoja wa watuhumiwa alikuwa bado mikononi mwa polisi kwa kutokamilisha taratibu za dhamana hiyo akiendelea kumsubiri mdhamini wake aliyechelewesha barua ya udhamini.
 
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo amesema kesi yao itatajwa tena Februari 12, 2015


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo