Hofu imetanda kwa wazazi wa watoto ambao wanasoma shule za msingi za Kabasa A na B Wilaya ya Bunda, Mara baada ya kuibuka kwa ugonjwa wenye dalili za kupanda ‘mapepo’ ambao unawaathiri wanafunzi wa kike pekee.
Kutokana na ugonjwa huo kuhusishwa na
imani za kishirikina uongozi wa Wilaya uliwataka viongozi wa kijiji
kukaa na wazee wa kimila ili kumaliza tatizo hilo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya hiyo,
Boniface Maiga alisema Serikali haiamini ushirikina, kwa kuwa tatizo
limeanzia kwenye jamii basi jamii hiyo hiyo inapaswa kumaliza tatizo
hilo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kabasa B alisema ugonjwa huo ulianza kati ya January 21 na 28 huku wakidhani kuwa ugonjwa huo ni Malaria.