Bibi kizee anayekadiliwa kuwa na umri wa
miaka 70 asiyejulikana jina wala makazi yake ameanguka akiwa hajavaa
nguo yoyote nyumbani kwa mtu mkoa wa Shinyanga jambo ambalo limehusishwa
na imani za kishirikina.
Suzana Mwandu
ambaye ni mwenye nyumba ambayo kikongwe huyo alianguka anasema alimkuta
akiwa nje ya jiko lake ambapo baada ya kumsemesha bibi huyo alizinduka
na kuanza kuongea vitu visivyoeleweka ambapo mashuhuda walihisi kwamba
ni mshirikina.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, Waziri Issa
amekiri kuwepo kwa tukio hilo ambalo lilikusanya umati wa watu ambapo
muda mfupi baadaye Polisi walifika na kumchukua ili kumnusuru bibi huyo
kupigwa na wananchi wenye hasira.