
Tume
imesikitishwa na matukio yaliyotokea tarehe 27/01/2015 huko Mbagala
Wilaya ya Temeke Dar-es-Salaam, matukio ambayo yameoneshwa na Kituo cha
Televisheni cha “Channel Ten” ambayo yameashiria uvunjifu wa haki za
binadamu.
Mnamo
majira ya saa kumi na robo hadi kumi na nusu jioni, Kituo cha TV cha
“Channel Ten” kilirusha picha zilizoonesha kupigwa na Polisi baadhi ya
wananchi waliokamatwa kwa kile kilichoelezwa kushiriki mkutano wa Chama
cha Wananchi (CUF) uliosemekana kuwa si halali.
Tume tayari imeanza kuchunguza tukio hilo na taarifa kamili itatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.
Bahame T. M. Nyanduga
MWENYEKITI