Ni kweli Matonya aliwekewa madawa kwenye pombe? Alewa na kukutwa vichakani hajitambui



Hitmaker wa ‘Anita’ Matonya aliwekewa vitu vinavyohisiwa kuwa ni madawa kwenye pombe aliyokuwa akinywa, kwa mujibu wa Rich One ambaye ni jirani yake.

Picha ya Matonya inayomuonesha akiwa amelala vichakani hajitambui ilisambaa wiki hii kwenye mitandao ya kijamii kiasi cha watu kuzusha kuwa amefariki dunia.
 
Rich alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM  kuwa tangu afahamiane na Matonya hajawahi kumuona amekunywa pombe hadi kufikia hatua ya kupoteza.
 
“Nina imani kuwa washkaji waliokuwa naye walimwekea,” alisema rapper huyo. Bado Matonya hajaweza kuzungumzia skendo hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo