MWINJILISTI ALIYEMBAKA MTOTO WA MIAKA 16 ATUPWA JELA MIAKA 30 HUKO TABORA

MAHAKAMA ya Mkoa wa Tabora i m e m h u k u m u Mwinjilisti wa Kanisa la Menonite Ipuli Manispaa ya Tabora, kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji wa msichana wa miaka 16.

Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora, Joctan Rushwela alisema kifungo hicho kiwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.

Aliyetiwa hatiani kwa kosa la kubaka msichana huyo (jina tunalihifadhi ) ni Furaha Muhama (49), mkazi wa Misha Manispaa ya Tabora baada ya kupatikana na hatia ya makosa mawili.

Hakimu Rushwela alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, hakuwa na shaka yoyote ndio maana mahakamani ikafikia uamuzi wa kutoa kifungo hicho kwa mshitakiwa huyo.

Hakimu huyo alisema kwamba kitendo kilichofanywa na mwinjilisti huyo kwa muumini wake ni kinatishia amani waumini, ambao watakosa imani na watoa mahubiri.

Alisema kwamba kitendo kama hicho hakiwezi kuvumilika na mtandao wa sheria hasa Mahakama kutokana na vitendo vya aina hiyo kukithiri katika jamii.

Mahakama hiyo ilitoa hukumu kwa makosa mawili, ambapo kosa la ubakaji kifungo miaka 30 na kumtorosha mtu kwenye himaya ya wazazi kifungo miaka 5, lakini makosa yote yanakwenda na kifungo kitakuwa miaka 30 jela.

Licha ya kutolewa kwa hukumu huyo, mshitakiwa hakuonesha kuumizwa na kosa hilo hata baada ya kutakiwa kusema chochote, alisema atakata rufaa tu hakimu huyo atakapotoa hukumu yake.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mwendesha mashitaka wa Serikali aliomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa huyo ili aweze kujutia kosa alilolifanya.

Awali mwendesha mashitaka wa serikali, Iddy Mgeni aliiambia mahakama hiyo kwamba Aprili 24 mwaka huu katika kijiji na Kata ya Ibambo wilaya ya Uyui mkoani hapa, mshitakiwa alikamatwa kwa makosa mawili ya ubakaji na kumtorosha mtu kwenye himaya ya wazazi wake.

credits kwa habari leo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo