Makamba: Enzi za ushindi wa kishindo CCM zimepita

Siku chache baada ya matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuonyesha kuwa CCM, imeporomoka, Mbunge wa Bumbuli, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amewataka wanachama wa chama hicho kujiandaa kisaikolojia kwa matokeo yoyote yanayoweza kutokea katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.
 
Wana-CCM wanatakiwa kujiandaa kisaikolojia kwani walizoea ushindi wa asilimia 90 au 80 (wa kishindo), huu ulikuwa ushindi wa nyuma. Tusishangae tukipata ushindi wa asilimia 50, 60, 57 au 70 ni kitu cha kawaida kutokana na kukua kwa demokrasia hususan ushindani wa vyama vingi vya siasa kuanza kuimarika:-Makamba
 
Kauli hiyo ya Makamba imekuja wakati matokeo ya serikali za mitaa yakionyesha kuwa CCM imeporomoka kutoka ushindi wa asilimia 91.7 mwaka 2009 hadi 79.8 katika uchaguzi wa mwaka jana na upinzani ukipanda kutoka asilimia nane mwaka 2009 hadi takriban 20 mwaka jana.
 
Akizungumza jana katika mahojiano na kipindi cha ‘Power Breakfast’ cha Redio ya Clouds na baadaye kufafanua alisema matokeo ya uchaguzi huo ni ishara kwamba kwa umri wa miaka 22 sasa, mfumo wa vyama vingi vya siasa umeanza kuimarika.
 
Hata ushindi wa asilimia 81 tulioupata katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa bado ni mkubwa na hata kama tungepata asilimia 70 haupunguzi uhalali wa uongozi. Kusema CCM itang’oka madarakani, hapana, bado wananchi wanakiamini tena sana:-Makamba.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo