SIKU moja baada ya kuachiwa kwa dhamana, kutokana na kesi
inayomkabili ya kudaiwa kuwachochea wafanyabiashara wasilipe kodi ya
Serikali, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Nchini, Johnson Minja
(34), amewataka wafanyabiashara kufungua maduka yao na kuendelea na
biashara.
Pia, amewataka kuendelea kushirikiana na Mamlaka ya Mapato nchini
(TRA) kuhakikisha wanatimiza wajibu wao. Alitoa kauli hiyo juzi wakati
akiachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma Mjini.
Alisema yeye hataki kuzungumzia tuhuma zinazomkabili kwa kuwa zipo
mahakamani. Hata hivyo, alisema kwamba yeye hajawahi kuchochea
wafanyabiashara kuacha kulipa kodi na mara zote amekuwa akiwahimiza
kulipa kodi, kwani ni wajibu wao.
“Mimi ninao utetezi…na serikali inao ushahidi ukweli utajulikana
mahakamani.. siwezi kuongelea hayo,” alisema alipokuwa Lakini, alisema
ni vyema wafanyabiashara wasitishe mgomo na kutoa ushirikiano kwa
serikali wakati mazungumzo ya kawaida kati ya wafanyabiashara na
serikali kuhusu matatizo yanayokwamisha ulipaji kodi yakiendelea.
Aidha, aliitaka TRA kushirikiana na wafanyabiashara ili kuondoa
vikwazo, vinavyokwamisha ulipaji kodi wenye tija kwa serikali na kwa
wafanyabiashara.
Juzi wafanyabiashara wengi katika mikoa mbalimbali nchini ikiwamo Dar
es Salaam, Mwanza, Tanga, Iringa na Dodoma walifunga maduka wakitaka
kujua hatima ya Mwenyekiti wao, huku wakilalamikia mashine za kodi za
kielektroniki.
Katika kesi iliyopo mbele ya Hakimu Mkazi Rebecca Minja, mtu huyo
anadaiwa kuwa Septemba 6, mwaka jana katika Chuo cha Mipango Dodoma,
akiwa kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania
aliwashawishi Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Dodoma wasilipe kodi.
Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa Septemba 6, mwaka jana katika
Chuo Cha Mipango mshtakiwa aliwapa maelekezo wafanyabiashara wa Dodoma,
wasitumie mashine za kodi za kielektroniki (EFD) za Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), ambazo zilitengenewa kwa ajili ya kuwezesha kukusanywa
kwa kodi. Mshitakiwa alikana mashtaka hayo.
Alisomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali, Godfrey Wambali. Na
katika hatua nyingine, wenye maduka mkoani hapa wameyafungua, ingawa
walisema kwamba bado hawapendezwi na mashine hizo, ambazo hazijali mtu
akirudisha kifaa kilichonunuliwa.
Walisema mashine hizo, zina matatizo mengi yanayotia hasara
wafanyabiashara na kwamba serikali inastahili kuwasikiliza na wao pia.
Wakati huo huo, Frank Leonard kutoka Iringa anaripopti kuwa
wafanyabiashara wa maduka wa wilaya za mkoa wa Iringa, wameitaka
serikali kusikiliza na kuyafanyia kazi madai yao ili kuondokana na
mivutano ya mara kwa mara inayodhoofisha huduma kwa wananchi.
Juzi asubuhi walifunga maduka yao, wakilenga kuvishinikiza vyombo vya dola kumuachia Mwenyekiti wao wa Taifa, Johnson Minja
aliyekamatwa Dar na kisha kupandishwa kortini Dodoma.
aliyekamatwa Dar na kisha kupandishwa kortini Dodoma.
Lakini, baada ya Minja kuachiwa huru, baadaye juzi jioni,
wafanyabiashara hao walitoa tangazo kwa wenzao wote kuendelea na
biashara zao kama kawaida.
Akihojiwa, Katibu wa wafanyabiashara hao wa mkoa wa Iringa, Jackson Kalole alisema tuhuma zinazotolewa dhidi ya mwenyekiti
wao wa taifa ni za uzushi. Alisema pamoja na kulipa kodi, wafanyabiashara wanayo malalamiko yao, yanayotaka mfumo wa ulipaji kodi ubadilishwe.
“Tunataka kodi ilipwe kwenye faida, isikatwe kutoka kwenye mtaji na hilo ndio moja ya malalamiko yetu makubwa. Lakini
tunataka pia kodi zote zinazoanzishwa na serikali, halmashauri zisianze kutoza kabla ya kupata maoni kutoka kwa wadau,” alisema.
tunataka pia kodi zote zinazoanzishwa na serikali, halmashauri zisianze kutoza kabla ya kupata maoni kutoka kwa wadau,” alisema.
Alisema wafanyabiashara wamekuwa wakigoma mara kwa mara kwa sababu
serikali imeacha mianya mikubwa, inayowapotezea mapato na kufukuzana na
wafanyabiashara ndogo.