Kauli ya Zitto Kabwe baada ya Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Sospeter Muhongo Kujiuzulu


Kufuatia hatua  ya Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Sospeter Muhongo kujiuzulu katika  nafasi  hiyo ya  uwaziri,  mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mh Zitto Kabwe amepongeza uamuzi huo wa Prof Muhongo ambapo amesema kuwa hatua hiyo ni heshima kubwa kwa bunge.
 
"Napenda kuchukua nafasi hii kutambua busara aliyochukua ambayo naamini itasaidia harakati za kujenga demokrasia yenye uwajibikaji. 
 
"Naamini uamuzi wa Ndugu Muhongo umewezesha kulinda heshima ya Bunge na maazimio yake. Kwa muda mfupi alioongoza Wizara hiyo, Ndugu Muhongo ameweza kuongoza mabadiliko kadhaa muhimu ya kiutendaji katika wizara hiyo na taasisi zake. 
 
"Hata hivyo, nafasi ya Wizara aliyokuwa anaongoza katika suala la Tegeta Escrow imemtia doa kubwa ambalo ilikuwa lazima awajibike. 
 
"Naamini Rais Kikwete atamteua mtu mchapakazi na makini zaidi atakayeweza kuendeleza yale mazuri ya Ndugu Muhongo na kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza." Amesema Zitto kupitia ukurasa wake wa Facebook.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo