Katika taarifa kubwa mbili zilizoripotiwa na kituo cha ITV kwenye habari za saa siku ya Desemba 02, ni kuhusu kile kilichosemwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya PAC
na Dk. Khamis Kigwangala kuhusiana na wananchi kukosa imani na Serikali
na habari nyingine ni kuhusu Kikao cha Bunge la Vijana Dodoma.
Dk. Kigwangwala: Wananchi wanakosa imani na Serikali
Tabia ya Serikali kutochukua hatua kali
za kisheria kwa viongozi wanaobainika kuchukua mali ya umma inawafanya
wananchi kukosa imani na Serikali yao na pengine kusababisha kutoweka
kwa amani kwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuvumilia shida wakati anaona
watu wachache wakigawana mali na kuendelea na nyadhifa zao.
Akizungumza hayo Kigwangala amesema; “…Haya
hayakubaliki na hatuwezi kukubali kundi la watu wachache kutoka kizazi
kingine wamepewa dhamananchi imewapa heshima kubwa wanaendelea kuiba
wakati na sisi tupo, waadilifu tuendelee kutazama jambo hilo tumesema
hapana hatutoruhusu mtu atumie pesa zetu, halafu afukuzwe tu kazi
yaishie hapo aende kutanua huko mjini nasema aendelee kutumia pesa
zake … aende akaishi kwa raha huko nje…“
Kikao cha Bunge la Vijana Dodoma
Katika taarifa nyingine ITV imeripoti
kuanza kwa Bunge la Vijana ambapo, Bunge la Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania, limeandaa Bunge maalum la Vijana linalofanyika kwa mara ya
kwanza chini ya Bunge la Tanzania mjini Dodoma kwa siku tatu.
Bunge hilo linajumuisha vijana 150
kutoka vyuo vikuu nchini ili kuwajengea uwezo wa kushiriki kikamilifu
katika masuala ya Kibunge na Siasa kwa kutambua wao ni Viongozi wa
kesho.
Akiwa katika eneo la viwanja vya Bunge, mmoja ya vijana hao amesema “…
Kwanza kabisa kwa upande wangu wa Serikali nzima ni kufuata kanuni
ambazo zimewekwa kuendesha Bunge hili la Vijana, pili ni kufuata yale
ambayo kambi nzima ya Serikali imepanga kusimamia kile ambacho
kinatupeleka katika mchakato mzima na mswada mzima wa Sheria ambayo
tunayotaka kuitunga…”