Rais wa Serikali ya wanafunzi katika chuo kikuu cha Dodoma Udom
Masatu Kyabwene amekiri kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wa vyuo vya
elimu ya juu Dodoma kujihusisha na biashara ya ukahaba kutokana na
kukosa mikopo.
Alitoa taarifa hiyo kutokana na kuwepo kwa taarifa ya kuwepo kwa
wanafunzi wanaojihusisha na biashara za ukahaba katika kumbi mbalimbali
za starehe.
“Kuna baadhi ya wanafunzi chuoni kwangu wana maisha magumu sana
kutokana na kukosa mkopo,wakati mwingine wananifuata mimi na kunielezea
shida zao ili niwasaidie,wengine ni yatima hawana baba wala mama wa
kuwalipia ada,siyo siri maisha ya wanafunzi hawa ni magumu sana”alisema.
Alisema anachofahamu wanaofanya biashara hiyo si wanafunzi wa Udom
pekee bali ni wote wanaotoka katika vyuo mbalimbali Mkoani humo na hata
sehemu nyingine hapa nchini.