Mgombea CCM, mpigakura wafariki dunia ghafla


Mgombea uenyekiti kupitia CCM Mtaa wa Swea, Kata ya Mkolani, Nyamagana, Mwanza, Pius Mihayo amefariki dunia ghafla akiwa mtaani kwake, muda mfupi baada ya kupiga kura.
 
Msimamizi wa uchaguzi huo, Halifa Hida alisema mgombea huyo alifariki dunia ghafla akiwa kwenye mtaa wake wa Swea na chanzo cha kifo hicho hakijajulikana... “Sasa kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi, tutatangaza matokeo ya wajumbe na nafasi za wagombea wa viti maalumu, nafasi ya uenyekiti haitatangazwa hadi taratibu nyingine za uchaguzi zitakapoandaliwa,” alisema Hida.
 
Mkoani Arusha msongamano wa kupiga kura, katika kituo cha Mbauda, Kata ya Sombetini unadaiwa kusababisha kifo cha mtu aliyetambulika kwa jina la Suleiman Bakari.
 
Tukio hilo lilitokea saa tatu asubuhi katika kituo hicho ambacho kilikuwa kimefurika watu. Mjomba wa marehemu, Ramadhani Athumani alisema kifo hicho kimewashtua kwani marehemu hakuwa mgonjwa.
 
“Marehemu alikuwa ni kinyozi na baada ya kupiga kura alianguka ghafla,” alisema Athumani .


Wagoma kupitishwa bila kupingwa
Vituko vya uchaguzi vimeendelea katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambako pamoja na mambo mengine, baadhi ya wagombea wa CCM waliopita bila kupingwa wameamua kujitoa baada ya kutishiwa maisha.
 
Tukio la wagombea kutishiwa maisha lilitokea wilayani Busega, Mkoa wa Simiyu ambako uchaguzi huo ulikumbwa na vurugu mbalimbali. Taarifa zilizotolewa na Mkuu wa wilaya hiyo, Paul Mzindakaya zinasema wagombea kupitia CCM katika Mji wa Lamadi, walijiondoa dakika za mwisho.
 
Hatua hiyo inadaiwa imetokana na wagombea hao kutishiwa maisha, kuchomewa moto nyumba zao na kwamba kutoka kwa wafuasi wa chama kimoja cha siasa.
 
Mzindakaya alisema wagombea wa Chadema Kijiji cha Lamadi walienguliwa kutokana na kutokidhi vigezo baada ya kuwekewa pingamizi, huku wakisalia wa CCM pekee.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo