VITUO VYA TELEVISHENI NA REDIO KURIPOTI HABARI ZA MAHAKAMA WAKATI KESI IKIENDELEA LAIVU

Usiache kupitia undani wa Stori kubwa muhimu kwenye Magazeti ya Tanzania leo December 4,2014
Mahakama inaangalia uwezekano wa kuruhusu vyombo vya habari kurekodi picha na sauti kuwezesha vituo vya redio na Televisheni kuripoti habari za mahakama wakati kesi zinaendelea.

Jaji Mkuu Othman Chande alisema mahakama inajifunza kutoka kwa nchi zinazoruhusu vituo vya redio na televisheni kuripoti habari wakati kesi inaendelea.

Alisema utaratibu huo utaanza kwa kuripoti kesi za madai zenye mvuto kwa jamii na kwamba utaratibu mzima unapaswa kufanyika kwa umakini mkubwa baada ya mahakama na vyombo vya habari kukaa pamoja juu ya maadili,uhuru na mipaka ya muhimili ili kuondoa migongano wakati wa kuandika na kuripoti habari za mahakama kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Hivi sasa waandishi wa habari hawaruhusiwi kupiga picha za video wala kurekodi sauti wakati kesi zikiendelea badala yake wanaruhusiwa kuandika habari hizo kisha kuripoti kile walichoandika bila kuonyesha mwenendo mzima wa kesi kwa kutumia sauti na picha za video.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo