skip to main |
skip to sidebar
SOMA HII SEHEMU YA PILI KUHUSU KUFUKUZWA KWA KOCHA MAXIMO WA YANGA
Mwandishi wa habari za michezo Saleh Ally (salehjembe.blogspot.com)
ameripoti kwamba kocha Marcio Maximo ambae amechukua nafasi kwenye
vyombo vya habari baada ya taarifa kwamba katimuliwa kwenye club ya
Yanga, amewashangaza wengi baada ya kuibuka na kuendelea kuifundisha
Yanga mazoezini.
Kocha huyo amefanya hivyo December 17 & 18 ikiwa ni sehemu ya
kuonyesha hatambui suala la kuondolewa kwake kazin ingawa tayari
alishafanya mazungumzo na uongozi wa Yanga kuhusiana na hilo, taarifa
zinaeleza bado hajakabidhiwa barua rasmi.
Kocha huyo mbrazil na msaidizi wakeLeonardo Neiva waliendelea na kazi
yao kama kawaida kwenye wwanja wa shule ya sekondari ya Loyola huku
tayari kocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi
akiwa ameshawasili Dar es Salaam kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Mbrazil
huyo.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi