SERIKALI YATANGAZA KIAMA, SASA KUWATAJA HADHARANI WEZI WA DAWA ZITOLEWAZO NA MSD

Serikali imesema itawataja hadharani watu wote wanaodaiwa kujihusisha na wizi wa dawa zinazonunuliwa na serikali kupitia bohari kuu ya madawa (MSD) ili waweze kutambuliwa na wananchi, ambao wamekuwa  wakichangia ukosefuwa dawa katika vituo vya afya na hosipitali za serikali hapa nchini.

Hayo yamesemwa na katibu mkuu wizara ya afya na ustawi wa jamii, Dk Dornald Mmbando wakati wa ukaguzi wa kituo cha afya kijiji cha Msoga kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani, ambapo amesema tatizo la dawa limekuwa likiongezeka siku hadi siku kutokana na baadhi ya watendaji na watumishi wa serikali wasio waaminifu.
 
Dkt Mmbando amesema kuwa, serikali imejipanga kukabilina na magonjwa ya mlipuko kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya magonjwa mapya yanayoibuka na kuitikisa dunia, ambapo amewaomba wanainchi kutoa taarifa pale wanapo muona mtu mwenye dalili za ugonjwa wanaoutilia shaka ikiwemo ugonjwa wa Ebola.
 
Mbunge wa jimbo la Chalinze mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amisema kuwa, tatizo la upotevu wa dawa katika zahanati na vituo vya afya katika jimbo la Chalinze mkoani Pwani, ni kubwa kukilinganishwa na upatikanaji wa dawa, jambo linalo athiri utoaji wa huduma za afya, na kuleta manung'uniko toka kwa wanainchi wanapoenda kupata huduma kwenye vituo vya afya na zahanati katika jimbo la Chalinze.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo