Matokeo ya uchunguzi wa mwili wa mchezaji soka kutoka nchini
Cameroon, Albert Ebosse aliyefariki nchini Algeria miezi minne
iliyopita yamebaini aliuawa baada ya kuvamiwa na kupigwa katika eneo la
kubadilishia jezi na wala hakuuawa kwa kupigwa na kitu katika kichwa
chake kama ilivyokua imeripotiwa hapo awali.
Mchezaji huyo aliyekua alikiitumikia klabu ya JS Kabylie alifariki mwezi Agosti baada ya timu yake kufungwa.
Matokeo ya uchunguzi ulifanywa na serikali ya nchini Algeria
yalibaini kwamba mchezaji huyo wa aliyekua na umri wa miaka 24 aliuawa
baada ya kupigwa na kitu katika sehemu ya nyuma ya kichwa chake.
Lakini uchunguzi uliofanywa na mtaalam anayechunguza chanzo cha kifo
kufuatia ruhusa iliotolewa na familia yake, umeonyesha kuwa kifo chake
kimetokana na uvamizi wa kikatili dhidi yake katika eneo la kubadilisha
jezi.
Wakati huo, waziri wa michezo nchini humo Algeria, Mohammed Tahmi
alisema, Ebosse alifariki baada ya kupigwa na kitu katika kichwa, kisa
hicho kilichosababisha klabu hiyo ya Kabylie kupigwa marufuku kwa miaka
miwili katika mashindano yoyote ya barani Afrika na kulazimishwa kucheza
michezo yake ya nyumbani bila mashabiki.
Lakini matokeo ya uchunguzi wa Andre Moune yamesema kuwa kulikuwa na
mvutano wakati wa uvamizi huo, ambapo Ebosse alipigwa ngumi katika
kichwa chake ilioathiri fuvu lake la kichwa.
