Timu 16 zilizofuzu kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 huko Equatorial Guinea zimepangwa katika makundi manne usiku huu katika hafla ya upangaji makundi iliyofanyika jijini Malabo ambako fainali hizo zitafanyika .
Makundi hayo yanaonyesha kuwa timu mwenyeji Equatorial Guinea imepangwa kwenye kundi ambako itakuwa na timu za Burkina Faso , Gabon pamoja na Congo brazzavile .
Kundi B limejumuisha timu za Zambia , Tunisia , Cape Verde na Congo Drc , .
Kundi jingine ambalo ni kundi C lina timu za Ghana , Afrika Kusini, Senegal na Algeria huku Kundi D likiwa na timu za Ivory Coast, Guinea , Cameroon na Mali .
Michuano hiyo ambayo awali ilikuwa ifanyike nchini Morocco kabla ya kuhamishiwa nchini Equatorial Guinea itafanyika kati ya Januari 15 na Februari 8 mwakani.
Kundi A .
Equatorial Guinea
Gabon
Burkina Faso
Congo Brazzaville.
Kundi B
Zambia
Tunisia
Cape Verde
Congo Drc
Kundi C
Ghana
Afrika Kusini
Senegal
Algeria
Kundi D.
Ivory Coast
Cameroon
Guinea.
Mali.
Michuano hii itafanyika kwenye miji minne huko Equatorial Guinea ambako Kundi A litacheza mechi zake kwenye kituo cha kwanza ambacho kiko kwenye mji wa Bata , Kundi B litakuwa litakuwa huko Ebibeyin , Kundi C litachezea kwenye mji wa Mongomo na Kundi litakuwa kwenye mji mkuu wa Equatorial Guinea huko Malabo.