Mafundi uashi wawili wamegundua mabomu
manane ya kutupwa kwa mkono ambayo inasemekana yamekuwepo ardhini kwa
Zaidi ya miaka 10 Kigoma kwenye Kijiji cha Mabamba walipokuwa wakichimba
msingi wa nyumba ya Mganga wa Kituo cha Afya.
Mafundi hao wamesema baada ya kubaini
kuwepo kwa chuma ambacho hawakukitambua waliamua kutoa taarifa Polisi na
Jeshi la Wananchi JWTZ, ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Jafari
Mohamed amethibitisha kutoa kwa tukio hilo.
Kamanda huyo amesema wanaendelea
kuwahoji watu kadhaa ikiwemo Diwani wa wa Kata hiyo ambaye alikuwa
anaimiliki nyumba hiyo kabla ya kuiuzia Halmashauri ya Wilaya ya
Kibondo, Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Venance Mwamoto amesema huenda mabomu
hayo yaliachwa na wapiganaji wa kutoka Burundi walipokuwa nchini kama
Wakimbizi.