Mtu mmoja Afariki Dunia baada ya kulipuliwa na bomu alilotaka kuwarushia askari Polisi.....Tume yaundwa kuchunguza tukio hilo


Askari  polisi aliyejeruhiwa

Jeshi la polisi limeunda timu ya makachero kutoka makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es salaam  wakishirikiana na wa mkoa wa Ruvuma kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio la mtu mmoja aliyelipukiwa na bomu maeneo ya majengo mjini songea  na kujeruhi askari polisi wawili wakati akijiandaa kuwarushia  askari waliokuwa doria na kisha bomu hilo kumuua mwenyewe.
 
Hayo yameelezwa na kaimu mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Diwani Athumani aliyewasili mjini  Songea kwa helkopta kwa ajili ya tukio hilo ambalo mtu ambaye hajatambulika,   amelipukiwa na bomu na kufariki dunia  wakati akijaribu kuwarushia bomu askari waliokuwa doria na kujeruhi askari wawili PC Mselemu na WP Mariamu Lukindo  ambaye bado amelazwa hospitalini Songea.
 
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said  Mwambungu aliyemtembelea majeruhi Mariamu Lukindo  ameeleza kusikitishwa na tukio hilo ambalo ni la tatu katika mwaku huu likiwalenga  askari polisi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo