MUME AMPIGA BAKORA MKEWE HADI AKAFA, KISA KAENDA KUPIGA KURA

Suzan Luhende mkazi wa Jomu Kata Wilayani Shinyanga ameuawa kwa kupigwa na fimbo na mumewe baada ya kutokea ugomvi baina yao alipozuiwa kwenda kupiga kura juzi wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika nchini kote.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema kifo hicho kilitokana na ugomvi kati yao baada mume ambaye ni mfuasi wa CCM kumkataza mkewe kwenda kupiga kura.

“Wanandoa hawa huwa wanagombana mara kwa mara kwa vile wote wanakunywa pombe za kienyeji,”alisema mmoja wa mashuhuda.

Mwenyekiti wa Serikali za mitaa Cheyo Maganga alisema wakati tukio hilo linafanyika yeye alikua katika shughuli za uchaguzi na kwa sasa uchunguzi unaendelea kujua chanzo cha kifo chake.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo