Na MatukiodaimaBlog
.WANANCHI wa kitongoji cha Dodoma kijiji cha Amani wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kuondokana na kero ya maji safi na salama baada ya mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kuwatimizia ahadi yake ya vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 14. 5 kwa ajili ya kuvuta na kusambaza maji safi na salama ya bomba katika kitongoji hicho .
.WANANCHI wa kitongoji cha Dodoma kijiji cha Amani wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kuondokana na kero ya maji safi na salama baada ya mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kuwatimizia ahadi yake ya vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 14. 5 kwa ajili ya kuvuta na kusambaza maji safi na salama ya bomba katika kitongoji hicho .
Akishukuru kwa niaba ya wananchi
wengine wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa hivyo jana Bi Belinada
Mwenda alisema kuwa awali wananchi wapatoa zaidi ya 600 wa kitongoji
hicho ambacho kimeanzishwa na jamii ya wachimbaji wa madini ya
dhahabu ,walikuwa wakitumia maji machafu yanayotumika kuoshea madini
na kunyweshea mifuko .
Hivyo alisema kuwa msaada huo wa
maji safi na salama utasaidia kuwaepusha na magonjwa na milipuko kama
kuhara na mengine ambayo walikuwa wakiyapata kutokana na matumizi ya
maji yasiyo salama kwa afya ya binadamu kwa kipindi chote cha zaidi
ya miaka 10 sasa toka kitongoji hicho kilipoanzishwa mwaka 1992.
” Hakika tunakushukuru sana mbunge
wetu kwa kutusaidia msaada wa vifaa hivi kwa ajili ya maji …..toka
mwaka 1992 hadi leo tumekuwa tukiteseka kwa magonjwa mbali mbali na
hata baadhi yetu kupoteza maisha kutokana na matumizi ya maji
machafu ambayo tulikuwa tukitumia maji ambacho kimsingi yalikuwa ni
mabaki ya maji yanayobaki katika kunyweshea mifugo na kuoshea madini”
Bi Mwenda alisema wananchi hao mbali
ya kero kubwa ya maji ambayo walikuwa wakiipata ila bado walionyesha
uaminifu kwa mbunge wao kwa kuendelea kubaki ndani ya CCM hadi sasa
wanapotimiziwa ahadi yao hiyo kwa kitongoji hicho kuwa ni moja
kati ya vitongoji vyenye msimamo na mbunge wao kwa kutoviunga mkono
vyama vya upinzani .
” Kwa shida tuliyokuwa tukiipata kama
maeneo mengine leo wote tungekuwa tumejiunga na upinzani ila
tuliamini chama pekee ambacho kinaweza kutusaidia na CCM na ndio
sababu hatukuona sababu ya kujiunga na vyama vya upinzani
…..mheshimiwa mbunge wetu tunakuhakikishia kuwa kitongoji hiki hakuna
hata mwananchi mmoja ambae ni upinzani na wala hatuna mpango wa
kuhangaika na vyama sisi tutabanana hapa hapa CCM”
Akizungumza na wananchi hao mbunge Bw
Filikunjombe pamoja na kuwapongeza kwa kutojiunga na vyama vya
upinzani bado alisema kuwa ameguswa kutimiza ahadi yake kwa wakati
kutokana na mateso makubwa ambayo wananchi hao walikuwa wakiyapata
kwa kukosa huduma ya maji safi na salama .
Kwani alisema kuwa lengo la serikali
ya CCM iliyopo madakarani chini ya Rais Dr Jakaya Kikwete ni kuona
watanzania wanaendelea kuboreshewa mazingira ya maisha yao na hata
kupunguza baadhi ya kero zinazoweza kupunguzw kwa wakati uliopo na
ndio sababu ya yeye kama mbunge pia kuendelea kukimbiza kasi ya
maendeleo ya jimbo hilo la Ludewa na kamwe hatakubali kuona wananchi
wake wakiendelea kuteseka.
“Ndungu zangu wananchi wa kitongoji
hiki cha Dodoma katika kijiji hiki cha Amani nimewapenda sana na
ninyi wenyewe mnatambua kuwa mimi mbunge wenu nawapenda ….. hivyo
msaada huo leo ni utekelezaji wa ahadi yangu niliyoitoka miezi
michache iliyopita nikiwa kama mbunge wenu japo siku nilipotoa
ahadi hii baadhi yenu hamkuweza kuamini kama leo ingetekelezwa
…nawaombeni sasa tunzeni vema vifaa hivi na kutunza zaidi mazingira
ili kufanya chanzo cha maji kuendelea kuwa hai zaidi “
Mbunge Filikunjombe alivitaja vifaa
ambavyo amevitoa ni pamoja na bomba za maji ambazo zitasambazwa katika
kitongoji chote kutoka kwenye chanzo cha maji zaidi ya kilometa 20
hadi kwenye kitongoji hicho .
Kuhusu wafugaji wanaochungia mifugo
katika chanzo cha maji mbunge huyo aliwataka wananchi na viongozi
hao kuweka sheria ya kulinda chanzo hicho cha maji vinginevyo
hakutakuwa na maana ya kuwa na bomba za maji safi ambazo zitaingiliwa
na mifugo.