Ule msemo wa ng’ombe hazeeki maini au ule wa kiingereza ‘Old is Gold’ naweza kusema ni kama una ukweli kwa kulirejea tukio hili ambalo ni la aina yake.
Kijana wa miaka 29, Elliot Seymour
ambaye damu inachemka alijikuta katika wakati mgumu kwenye uliongo wa
mchezo wa ngumi pale aliposhindwa kujitutumua mbele ya mzee, kikongwe Mickey Rourke ambaye ni bondia wa zamani na pia muigizaji wa Holywood.
Katika pambano hilo ambalo lilifanyika
siku ya ijumaa Marekani, kwanza lilikuwa na kiingilio kikubwa, pili
lilikuwa na mvuto wa aina yake ambapo watu walihitaji kupata jibu kati
ya babu wa miaka 62 na jamaa wa miaka 29 nani atamshinda mwenzake.
Babu alimpiga Seymour kwenye round ya pili ya mchezo, amekuwa gumzo kubwa mitandaoni.