BAADA YA MUME KUKOSA KITOWEO CHA KUKU KRISMASI, AMFANYIA KITU MBAYA MKEWE

Kama ulifanikiwa kuisherehekea Christmas ya mwaka huu 2014 kwa amani basi ni heri kwako, kumbe wakati wengine wakisherekea kwa amani Sikukuu hii kubwa ya mwaka kuna sehemu ambazo hakukuwa na heri yoyote siku hiyo.
 
Story hii ya kusikitisha inatoka Kenya ambapo jamaa mmoja Daniel Imonje, alimpiga mke wake kwa shoka mpaka kufariki, majirani walioshuhudia wakisema eti kisa ilikuwa ni kitendo cha mke wake huyo kutomuandalia mume wake nyama ya kuku siku ya Christmas, badala yake akaandaa rosti ya nyama ya ng’ombe.

Ni wengi waliolaani  kitendo hicho kilichotokea Kijiji cha Shanderema, Kenya na mashuhuda wamesema Daniel alifanya unyama huo akiwa amelewa.

Mtuhumiwa anashikiliwa katika kituo cha Polisi cha Kakamega baada ya kufanya mauaji hayo kwa ajili ya uchunguzi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo