Azam FC Wamkana Amis Tabwe, Wasema Kikosi Chao Kimekamilika

Mkurugenzi wa ufundi wa klabu bingwa Tanzania bara Azam FC, Sadi Kawemba amesema walikua hawana mpango wowote na mshambuliaji kutoka nchini Burundi, Amis Tambwe ambae amejiunga na Dar es salaam young Africans baada ya kutemwa na klabu ya Simba katika dirisha dogo la usajili.

Kawemba amesema taarifa za Azam FC kumuhitaji Amis Tambwe zilikua zinavumishwa na vyombo vya habari lakini hawakuwahi kuonyesha hata dalili za kumsajili mshambuliaji huyo ambaye alimaliza msimu uliopita kwa kuibuka kinara wa upachikaji mabao kwenye ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Amesema kikosi chao kina wachezaji wa kutosha katika safu ya ushambuliaji na katika mapendekezo waliyoyapokea kutoka kwa kocha wao Joseph Marius Omog kupitia ripoti aliyoiwasilisha kwa viongozi mara baada ya kucheza michezo saba ya ligi kuu ya soka Tanzania bara kulikua hakuna ombi la kuongezwa kwa mshambuliaji.

“Tupo vizuri tunae Kavumbagu, nahodha wetu John Bocco anarudi hivi karibuni uwanjani, tuna Gaudence Mwaikimba, Kipre Tcheche, Khamis Mcha na bado kuna wachezaji ambao wana uwezo wa kucheza wakitokea pembeni na kusaidia mashambulizi hivyo hatuoni sababu ya kuongeza mchezaji mwingine.”

“Tabwe alikua anapendekezwa na watu tumsajili hususan mashabiki lakini tuliona hakuna nafasi ya kufanya hivyo kutokana na kuamini wapo wachezaji ambao wana uwezo wa kutusaidia katika michuano ya ligi kuu pamoja na ile ya klabu bingwa Afrika.” Amesema Kawemba.

Katika kipindi cha dirisha dogo la usajilia mbacho kilifungwa rasmi mwanzoni mwa juma hili Azam FC imewasajili Pascal Wawa, Majwega na Amri Kiemba huku iliowaacha ni Ismail Diara raia wa Mali pamoja na Mhaiti Lionel Saint-Preux


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo