Spika wa Bunge la Afrika Mashariki EALA, Margaret Zziwa
amesimamishwa kazi na Wabunge wa Bunge hilo kwa kile kinachoelezwa kuwa
amekuwa akiendeleza ubaguzi kwenye ajira, ufisadi na pia hana uongozi
bora.
Katika mahojiano aliyoyafanya na kituo cha BBC
amekana madai hayo na kusema malumbano yanayoendelea ndani ya Bunge
hilo yanatokana na siasa za chuki baina ya Wabunge na kusababisha Bunge
hilo kutimiza majukumu yake.
Uchunguzi unafanyika ili kujua kama madai yaliyopelekea kumsimamisha yalikuwa na ukweli wowote.
Hapa nimekuwekea taarifa hiyo ambayo iliripotiwa na BBC, unaweza kubonyeza play kuisikiliza.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi