Mbunge James Mbatia alikuwa wa kwanza kuruhusiwa kuomba mwongozo huo; “…
Wizi huu na usambazaji wa taarifa ya ukaguzi maalum kabla
haijawasilishwa Bungeni ni vitendo vinavyotakiwa kukemewa na kutolewa
tamko kali na Bunge, hivyo basi kwa kutumia kanuni ya 51 ya kanuni za
Bunge toleo la mwaka 2013, naomba kutoa hoja Mheshimiwa Spika kwamba
Bunge lako lisitishe shughuli zake zilizopangwa kuendelea sasa, ili
Wabunge wapate fursa ya kujadili suala hili kwa kina na kutoa maagizo
yanayostahili kwa Serikali …”
Spika Anne Makinda akajibu; “…
Huyo aliyehusika ameshikwa na yuko mikononi mwa Polisi sasa hivi, ofisi
yangu ya Bunge imeshirikiana na Polisi kutomtoa yule mtu paka aseme
hivyo vitu alivyokuwa anavisambaza vimetoka wapi, ndio kazi inayoendelea
sasa hivi… hatuendeshi Bunge kwa kupiga kelele tuelewane, mtu yuko
ndani sasa hivi tunavyoongea tukipata taarifa ya Polisi ndio tutajadili
tunajadili nini”
Baadhi ya Wabunge hawakuridhishwa na majibu hayo ikiwemo Mbunge Tundu Lissu; “…
Mheshimiwa Spika umeridhika kuwa hili jambo linahusu haki za Bunge ndio
maana umempa Mheshimiwa Mbatia ruhusa ya kutoa hoja yake hatua
inayofuata… kwa mujibu wa hiki kifungu ni kuweka kipaumbele katika
shughuli nyingine zote za Bunge ili tujadili hili suala, sasa Mheshimiwa
Spika hili jambo hatujadili taarifa ya kamati tunajadili haya
yanayotokea ni vizuri Mheshimiwa Spika hili jambo lizungumzwe ili hii
hewa chafu inayoanza kujitokeza iwe clear…”
Spika Makinda akajibu; “…
Hili suala lingekuwa limetoka tuu mtaani na kuja humu ndani tungefanya
mnavyosema kwa sababu wote hatungekuwa informed, nyinyi hao na wenzenu
wengine ndio mliosaidia kumshika mtu aliyekuwa anasambaza, sasa Polisi
wanaendelea nasema wakishakamilisha hiyo Spika atapanga lakini bila
hivyo sasa tutafanya nini Polisi wanatafuta na sisi tunazungumza humu
ndani…”
Spika wa Bunge akampa nafasi Mbunge Ole Sendeka; “…
Kwa kuwa sii busara mimi kuendelea kulumbana na kiti chako kwa uamuzi
huo japo msimamo wangu ulikuwa ni ule, kwa mujibu wa maelezo uliyotoa
kama unavyojua jambo hili linahitaji kutendewa haki ni jambo linalohusu
uhalifu dhidi ya rasilimali za Nchi, hofu yangu Mheshimiwa Spika ni
kwamba siku hiyo wakati kamati itakapowasilisha ripoti hapa na ndio siku
ambayo Wabunge hao watapata nafasi ya kuiona ripoti ya CAG na ripoti
pia ya kamati ya PAC…“
Sasa
mashaka niliyonayo Mheshimiwa Spika ni muda gani Bunge lako litapata
nafasi ya kusoma kamati ya CAG kama vyote vitawasilishwa siku hiyo na
siku hiyo hiyo vikataliwa kujadiliwa wakati ambapo Wabunge hawajapata
uelewa mpana juu ya ripoti yenyewe, ni kwa nini sasa usielekeze katibu
wako wa Bunge ahakikishe kwamba ripoti hiyo inapatikana kwa Wabunge
mapema rasmi leo badala ya kupatikana huko mitaani, ili Wabunge waweze
kuisoma ripoti hii na vielelezo vyake ili waweze kuitendea haki ripoti
yenyewe, vinginevyo Mheshimiwa Spika utalazimika siku hiyo ripoti
itakapowasilishwa utupe siku nzima tena kwenda kujisomea na kupitia
vielelezo ili tuweze kuitendea haki ripoti yenyewe…”– Ole Sendeka.
Baada ya hoja ya Mbunge huyo, Anne Makinda akajibu; “…Hili tunafanya utaratibu kusudi mpate documenti mapema ili muweze kujadili hilo ndiyo tunakubali…”