Katika hali isiyokua ya kawaida Zahanati ya Matanga Manispaa ya Sumbawanga ina muuguzi mmoja tu ambaye anafanya kazi za kupima wagonjwa,kutoa dawa na kuzalisha kina mama kwa kutumia mwanga wa kibatari.
Muuguzi huyo Bruno Ntalyoka mwenye miaka 40 amefanya kazi kwa kipindi
cha mwaka mmoja baada ya daktari wa Zahanati hiyo kuhamishwa na yeye
kushikilia nafasi hiyo hadi leo.
Ntalyoka alisema alianza kazi mwaka1985 na hospitali hiyo ilikua na
daktari mmoja na yeye alikua akimsaidia lakini baada ya kuhamishwa yeye
alikua akifanya kazi zake zote.
“Nafanya kazi vizuri tu na hakuna tatizo lolote wala malalamiko
kutoka kwa wananchi,naamini haya yote yatakwisha baada ya Serikali
kuleta daktari mwingine.
Alisema inapotokea mama mjamzito anataka kujifungua husitisha
shughuli zote kwa wakati huo na kuanza kumuhudumia na kwa kawaida kila
mwezi huzalisha wajawazito18 ambao ni swa na wastani wa wanawake wawili
mpaka watatu kwa siku.
Alisema kazi hiyo inakua ngumu usiku kwa sababu Zahanati hiyo haina
umeme kwa muda mrefu sasa hivyo humbidi kutumia mwanga wa kibatari
kuwahudumia wakina mama hao